Nchimbi ahimiza uimarishaji mshikamano wa Kitaifa 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amehimiza jamii kuimarisha mshikamano wa kitaifa kama msingi wa maendeleo endelevu.

Dk.Nchimbi ametoa salamu za Sikukuu ya Pasaka katika Tamasha la Mtoko wa Pasaka lililoandaliwa na Wasanii wa Muziki wa Injili nchini lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Kupitia tamasha hilo,  amesisitiza umuhimu wa kudumisha mshikamano, amani, na upendo miongoni mwa watanzania na kuzingatia maadili mema.

Aidha, amewapongeza waandaaji wa hafla hiyo kwa kubuni na kutekeleza wazo la kuwaunganisha watu katika kusherehekea Pasaka, akibainisha kuwa matukio kama hayo yanachangia kuijenga jamii yenye mshikamano na matumaini kwa ajili ya mstakabali mwema wa taifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *