Kocha Etienne Ndairagije wa Polisi Kenya amesema Simba imepata mchezaji wa thamani kwa kumsajili Mohammed Bajaber, akieleza kuwa ana kipaji kikubwa cha kutengeneza nafasi na kufunga.

Simba inadaiwa imempa mkataba wa miaka miwili winga huyo wa kimataifa kutoka Kenya.
Bajaber amejiunga na Simba na kuondoka kwenye kikosi cha taifa cha Kenya kinachojiandaa na CHAN, huku Simba ikiwa kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.