Pamba Jiji imeachana na kocha Fred Minziro na ipo kwenye hatua za kumtangaza Francis Baraza kuwa mrithi wake.

Dodoma Jiji pia imeachana na kocha Mecky Maxime na inatafuta kocha mpya, huku taarifa zikidai huenda wakamtangaza Anicet Kiazayidi aliyeinoa Tabora United msimu uliopita.
Maxime anatajwa kuelekea Mtibwa Sugar iliyoibuka Ligi Kuu.