Pamba Jiji yamrejesha Kibailo, yatangaza benchi jipya la ufundi

Klabu ya Pamba Jiji imemrejesha beki wa kulia, Hassan Kibailo, kutoka Namungo FC, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Kibailo, ambaye amewahi kuchezea Coastal Union na Mtibwa Sugar, alikulia soka Mwanza na alichezea Pamba hadi mwaka 2021 kabla ya kusaka changamoto kwingine.

Pamoja na usajili huo, Pamba imemsajili kipa Arijifu Amour kutoka Azam FC na kiungo mshambuliaji raia wa Kenya, Siwa Oyugi, kutoka Kagera Sugar. Pia imemtangaza Themi Felix kuwa kocha msaidizi wa Francis Baraza na John Wawu kuwa kocha wa makipa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *