Prisons wapania kuifanya JKT ngao kubaki Ligi Kuu

Klabu ya Tanzania Prisons imeapa kuibuka na ushindi dhidi ya JKT Tanzania leo kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusalia Ligi Kuu.

Kocha Amani Josiah amesema wamejiandaa vizuri na kufanya mazoezi ya kimbinu, wakifahamu kuwa wanakutana na moja ya timu ngumu kwenye ligi. Mchezaji Wema Sadoki na kipa Sebusebu Samson pia wamesisitiza kuwa wanahitaji pointi zote tatu ili kufufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu.

Prisons ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24, huku zikiwa zimebaki mechi nne kumaliza msimu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *