Prisons yaanza mchakato wa kocha mpya, Bares na Odhiambo wamo

Klabu ya Prisons ipo katika mchakato wa kumpata kocha mpya kwa msimu ujao, ambapo majina ya Mohamed Abdallah ‘Bares’, Ahmad Ally, na Mkenya Patrick Odhiambo yanatajwa.

Kocha wa sasa, Amani Josiah, huenda akaachwa licha ya kuiokoa timu hiyo kupitia mechi ya mchujo dhidi ya Fountain Gate.

Mtendaji Mkuu wa klabu, John Matei, amesema klabu imeunda kamati ya usajili na inalenga kuwa na kikosi cha ushindani zaidi msimu ujao.

Prisons ilimaliza nafasi ya 13 kwenye Ligi Kuu kwa pointi 31 na ilinusurika kushuka daraja baada ya kushinda jumla ya mabao 4-2 dhidi ya Fountain Gate katika mechi ya mchujo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *