Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi (PSSSF) umeshirikiana na wadau wengine kurudisha matumaini ya watoto wagonjwa wa moyo na kwa akina mama wenye mimba hatarishi.

Kupitia waandaji wa CRDB 2025 Marathon, PSSSF imechangia kiasi cha shilingi milioni kumi zitakazowafikia wagonjwa husika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya CCBRT.
Katika mbio hizo ziliongozwa na Spika wa Bunge, Tulia Ackson, jumla wa wafanyakazi 100 walishiriki mbio hizo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ilala, Amina Kassim, amesema mchango huo ni sehemu ya kusaidia juhudi za Serikali kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa kila Mtanzania.
Ushiriki wa PSSSF tukio hilo ni kuunga mkono jitihada za wadau hasa benki ya CRDB kupitia kampeni yao ya Kasi Isambazayo Tabasamu kwa kuwa jamii bila ya afya bora maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana.









