Rais Dk. Samia akipokelewa na wakazi wa Dodoma baada ya kupokea tuzo ya Gates Goalkeeper Award

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema tuzo aliyokabidhiwa leo ya ‘Gates Goalkeeper Award’ inamaanisha kuwa, dunia imejua na kuona jitihada za Tanzania katika huduma za afya hususan za mama na mtoto.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 4, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akitokea Dar es Salaam.

Tuzo hiyo amepewa leo na Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation inayojihusisha na miradi inayolenga kuboresha afya, elimu na maendeleo ya kijamii hasa katika nchi zinazoendelea.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *