Rais Mwinyi: Hongera timu ya Simba kwa ushindi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewapongeza wachezaji wa timu ya Simba kwa ushindi walioupata katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, katika mchezo wa awali wa Nusu Fainali dhidi ya timu ya Stellenbosch Football Club ya Afrika Kusini.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo akiwa katika makaazi yake ya Ikulu Ndogo Migombani, Zanzibar, akifuatilia mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 20 Aprili 2025.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza timu ya Simba kwa kuuchagua Uwanja wa New Amaan Complex kuwa uwanja wao wa nyumbani na kueleza kuwa Serikali imefarijika na hatua hiyo, huku akiahidi kuendelea kuimarisha viwanja mbalimbali hapa Zanzibar.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *