Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa kiasi cha Tsh. Milioni 30 kwenye harambee ya ukarabati wa jengo la kanisa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flavian Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.