Rais Samia akiwasili Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa mkutano wa hadhara

TANGA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan, amewasili leo Februari 28, 2025, katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo maelfu ya wananchi wamefurika kumpokea na kushiriki katika mkutano wa hadhara.

Ziara hii ya kikazi inalenga kusikiliza kero za wananchi, kuzindua miradi ya maendeleo, na kuzungumzia agenda muhimu za taifa.

Wananchi wa Tanga wamejitokeza kwa wingi huku wakionesha shauku kubwa ya kumsikiliza kiongozi huyo wa nchi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *