Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariRais Samia aongoza Kikao Maalumu cha CCM

Rais Samia aongoza Kikao Maalumu cha CCM

Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) kilichofanyika jijini Dodoma, leo.

Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya chama na serikali, huku ajenda kuu ikiwa ni uteuzi wa wagombea wa nafasi za Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, kikao hicho pia kimefanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kama sehemu ya maandalizi kuelekea kuanza kwa vikao vya Bunge la 13, vinavyotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Katika vikao hivyo vya bunge vinavyotarajiwa kuanza mapema wiki ijayo, baadhi ya shughuli muhimu zitakazofanyika ni pamoja na wabunge wateule kula kiapo, uchaguzi wa Spika wa Bunge, pamoja na uteuzi wa jina la Waziri Mkuu litakalowasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge.

Kikao hiki maalumu cha Kamati Kuu ni cha kwanza kufanyika tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi chake cha pili kitakachokoma mwaka 2030.

Rais Samia aliapishwa Novemba 3, 2025, jijini Dodoma, mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Masaju, baada ya kutangazwa mshindi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, ambapo alishinda kwa asilimia 97.66 ya kura zote halali.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments