Rais Samia ashiriki Swala ya Eid El-Fitr Msikiti wa Mohamed VI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na waumini wa Kiislamu kuswali Swala ya Eid katika Msikiti wa Mohamed VI, uliopo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Ibada hiyo ni sehemu ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambapo waumini wa dini ya Kiislamu husherehekea Sikukuu ya Eid El-Fitr. Swala hiyo imefanyika tarehe 31 Machi 2025.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *