Bodi ya Ligi (TPLB) imekubali ombi la Ruvu Shooting kujiondoa Ligi Daraja la Kwanza, hivyo kuishusha hadi Ligi ya Mikoa na kuifungia kushiriki mashindano kwa misimu miwili.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya klabu hiyo kushindwa kumudu gharama za uendeshaji. Awali, ilikatwa alama 30 kwa kutofika uwanjani kwa michezo miwili, ikipoteza pointi 15 kwa kila mchezo na kupigwa faini ya Shilingi milioni 6.