Samia: Nimefurahi agizo langu la Haki Jinai linakwenda kufanyiwa kazi

“Waheshimiwa niungane na wote waliotangulia kumshukuru Mwenyezimungu. Kwa neema ha uhai na kutuwezesha kukutana tena. Nimefurahi kujumuika nanyi kwenye kilele cha wiki ya sheria na kuzindua shughuli za mahakama nchini kwa mwaka 2025. Mheshimiwa jaji Mkuu, nikiangalia kauli mbiu mliyokuja nayo mwaka huu inayosema Tanzania ya 2050, nafasi za taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya maendeleo. Kauli mbiu hii inanipa faraja kwamba agizo langu nililolitoa wakati napokea taarifa ya kamati ya kuangalia taasisi ya haki jinai sasa linakwenda kufanyiwa kazi,”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *