Sunday, March 29, 2026
spot_img
HomeMichezoSerengeti Girls yaichapa Tunisia ikisaka makali

Serengeti Girls yaichapa Tunisia ikisaka makali

TIMU ya soka ya Taifa ya Wasichana ya umri chini ya miaka 17 (Serengeti Girls), imeanza vema kambi yake ya mazoezi kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Tunisia kwenye Uwanja wa Mustapha Ben Jannet Monastir nchini humo leo.

Serengeti Girls imeweka kambi mjini Monastir nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu fainali za kombe la dunia zilizopangwa kufanyika Morocco baadae mwaka huu.

Timu hiyo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Bakari Shime ilitawala vipindi vyote vya mchezo na kufunga bao moja katika kila kipindi.

Yasinta Michael ndiye aliyeanza kufungua mlango wa ushindi kwa kufunga bao la kuongoza dakika ya 17 kabla Bahati Steven hajaongeza bao la pili dakika ya 53 na Aaliyah Juma kufunga bao la tatu katika dakika ya 90.

Serengeti inatarajiwa kucheza mechi ya marudiano na wapinzani wao hao Aprili 4 kabla ya kuelekea Gaborone siku inayofuata kucheza na timu ya Taifa ya Botswana katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Endapo itaiondoa Botswana, Girls itacheza na Afrika Kusini hatua inayofuata.

Serengeti Girls iliwahi kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 zilipofanyika India na kuweka historia kwa soka la wanawake kufuzu kombe la dunia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments