Serikali yazindua mfumo wa kidigitali wa kuuza jezi za Taifa Stars

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, amezindua rasmi mfumo wa mauzo ya jezi za timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa njia ya mtandao.

Mfumo huo unaolenga kuongeza upatikanaji wa jezi hizo kuelekea mashindano ya CHAN, unatekelezwa kwa ushirikiano wa Benki ya NBC, Vodacom na kampuni ya Sandalan. Mwana FA alihamasisha taasisi mbalimbali nchini kuruhusu wafanyakazi kuvaa jezi za Taifa Stars kama sehemu ya sare za kazi katika siku maalum.

Kupitia mfumo huo wa e-commerce wa NBC, watanzania wataweza kununua jezi hizo bila kufika dukani, jambo litakalorahisisha upatikanaji wake nchini kote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *