Shirikianeni na MSD kwenye mipango yenu kuboresha upatikanaji bidhaa za afya

Wadau wa Sekta ya Afya mkoani Kigoma, wametakiwa kushirikiana na MSD kwa ukaribu katika utekelezaji majukumu na mipango yao, Ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Rai hiyo imetolewa hii leo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rungwa wakati akifungua kikao kazi cha wadau na wateja wa MSD kutoka Mkoa wa Kigoma, kilichofanyika katika Ukumbi wa JM, ulioko Manispaa ya Tabora.

Rungwa amesisitiza kwamba Afya ndio msingi wa Maisha, hivyo kuwataka Wadau hao kushirikiana na MSD kwa ukaribu ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya na huduma kwa ujumla.

Amesema endapo wadau hao wa Afya wataishirikisha MSD kwenye malengo na mikakati yao, hatua hiyo itaisaidia MSD katika kuweka Mikakati ya pamoja sambamba na Wadau hao, ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya mkoani humo.

Rungwa amesisitiza kwamba iwapo MSD itapata taarifa na mahitaji sahihi ya kila mtoa huduma kwa wakati, mathalani ushirikishwaji kwenye miradi ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya, hakutakuwa na uhaba wa bidhaa za afya mara miundombinu hiyo ikamilikapo, kwani Wadau hao watakuwa wanazungumza lugha moja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *