Sunday, March 22, 2026
spot_img
HomeMichezoSimba yatoboa siri kwa Mwalimu

Simba yatoboa siri kwa Mwalimu

Klabu ya Simba imekiri iliwahi kufikiria kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Suleiman Mwalimu kutoka Wydad Casablanca ya Morocco, baada ya kocha aliyemsajili kuondoka, lakini dili hilo halikufanikiwa.

Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema iwapo usajili huo utatimia sasa, utakuwa ni hatua kubwa kwa mchezaji huyo kwani Simba ni timu kubwa zaidi ukilinganisha na Wydad.

Aidha, Ahmed alibainisha kuwa maandalizi ya Tamasha la Simba Day yanaendelea ambapo litafanyika Septemba 10 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya Septemba 7.

Tamasha hilo la 16 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, litakuwa na uzinduzi wa wachezaji wapya wa klabu hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments