Simiyu yakusanya milioni 300 faini kwa udanganyifu wa mizani ya pamba

Na Mwandishi Wetu
Mkoa wa Simiyu umekusanya zaidi ya Shilingi milioni 300 kama faini kwa vituo vya ununuzi wa pamba vilivyobainika kuchezea mizani ya kidigitali kwa lengo la kuwapunja wakulima msimu huu.


Mkuu wa Mkoa, Anamringi Macha, alisema faini hizo ni matokeo ya msako wa kushtukiza katika wilaya za Itilima na Busega, baada ya malalamiko kutoka kwa wakulima.


Katika vituo 300 vilivyobainika na kasoro, wafanyakazi 15 walitozwa faini na wengine wanakabiliwa na mashtaka ya udanganyifu. Mizani hizo, kati ya 800 zilizopo mkoani humo, zilibadilishwa baada ya kurekebishwa.

Macha alitoa onya kali kwa makarani wanaochezea mizani na kuwataka kuacha tamaa ya kuwanyonya wakulima.
Amesema serikali inalenga kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 140,000 hadi 500,000 kwa mwaka kwa kuimarisha utoaji wa pembejeo mapema na ushauri wa maofisa ugani.
Mkoa wa Simiyu unaongoza kitaifa kwa uzalishaji wa pamba, ukiwa na asilimia 60 ya uzalishaji wote nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *