Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah raia wa Ghana, kwa mkataba wa miaka miwili. Dili hilo lilikamilika juzi usiku kwa kusainiwa kwa njia ya kielektroniki nchini Ghana, huku ada ya usajili ikifichwa.

Sowah anatajwa kuwa mchezaji wa pili kwa mshahara mkubwa ndani ya Simba, nyuma ya Steven Mukwala. Kocha Fadlu Davids ndiye aliyependekeza usajili wake, akimuelezea kama mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania.
Akiwa na Singida Black Stars, Sowah alifunga mabao 13 kwenye Ligi Kuu, akimaliza nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji nyuma ya Jean Ahoa wa Simba aliyefunga mabao 16.
Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, hakuthibitisha moja kwa moja, lakini alisema amefurahishwa na taarifa hizo na kuomba dua dili hilo likamilike.