Sunday, March 22, 2026
spot_img
HomeMichezoSPUTANZA: Malalamiko ya wachezaji yamepungua

SPUTANZA: Malalamiko ya wachezaji yamepungua

Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania (SPUTANZA), Mussa Kisoki, amesema malalamiko ya wachezaji kuhusu mikataba na uhamisho yamepungua kutokana na kuongezeka kwa uelewa wa wachezaji na viongozi.

Amesema pia hatua ya TFF kuwalipa wachezaji wanaodai vilabu kupitia fedha zinazotolewa kwa klabu husika imepunguza migogoro.

Aidha, SPUTANZA imejiunga na Chama cha Wachezaji wa Dunia kinachotambuliwa na FIFA kwa kanda ya Afrika, hatua itakayosaidia kubadilishana uzoefu na kuimarisha vyama vya wachezaji.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments