Tabora United imesema iko tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Yanga na hawaogopi wapinzani wao, wakisisitiza kuwa mpira ni dakika 90.

Msemaji wa klabu hiyo, Christina Mwagala, amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wanataka kurudia ushindi wa 3-1 walioupata kwenye mzunguko wa kwanza.
“Baada ya kushindwa kusonga mbele kwenye Kombe la FA, tunataka kufuta machozi kwa kuifunga Yanga. Tupo tayari na tunahitaji pointi tatu,” alisema.
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa, hasa ikizingatiwa matokeo ya mzunguko wa kwanza ambapo Tabora United iliwashangaza Yanga kwa ushindi wa 3-1.