Tabora United yamtimua Kocha Genesis Mang’ombe

Klabu ya Tabora United imemfuta kazi kocha Genesis Mang’ombe, raia wa Zimbabwe, ikiwa ni chini ya mwezi tangu aanze kuinoa timu hiyo. Kocha huyo alikuwa amerithi mikoba ya Anicet Makiadi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Charles Obiny, amesema Mang’ombe ameondolewa kutokana na ukosefu wa uzoefu na uwezo mdogo wa kiufundi. Alieleza kuwa hata mazoezi ya kocha huyo hayakuwa na tija, na hata Mang’ombe mwenyewe alikiri kushindwa.

Chini ya Mang’ombe, Tabora ilipoteza mechi nne mfululizo, ikiwa ni pamoja na kichapo cha 3-0 kutoka kwa Mashujaa FC. Hii inamfanya kuwa kocha wa tatu kuondoka Tabora msimu huu, baada ya Francis Kimanzi na Anicet Makiadi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *