TANESCO: Maboresho ya miundombinu hayataathiri wananchi kwa siku sita mfululizo

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi kuhusu maboresho ya miundombinu yatakayofanyika kuanzia Februari 22 hadi Februari 28, 2025, likisisitiza kuwa maboresho hayo hayataendelea kwa siku sita mfululizo na hayatasababisha athari kubwa kwa wananchi.

Katika taarifa yake, TANESCO imeeleza kuwa maboresho hayo yatafanyika katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusafirisha Umeme cha Ubungo, ambapo kuna uwezekano wa kuathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Pwani.

Hata hivyo, shirika hilo limewahakikishia wananchi kuwa maboresho hayo yatatekelezwa kwa utaratibu wa kuzuia usumbufu mkubwa, hivyo wasiwe na hofu. TANESCO pia imeeleza kuwa inafanya kila jitihada kuhakikisha athari zitokanazo na maboresho hayo zinabaki kuwa ndogo kadri inavyowezekana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *