Tanzania yajipanga kwa Miss World 2027

Ulikuwa wakati munawari na mujarabu sana leo visiwani Zanzibar Rais, mwanamaono, kiongozi thabiti na mwanamageuzi asiyechoka Dk. @samia_suluhu_hassan alipozialika sekta mbili za @wizara_sanaatz na @wizarayamaliasilinautalii kushiriki mazungumzo na Kamati ya Mashindando ya Unyange Duniani (Miss World) waliofika nchini wakiwa na Rais wa Kamati hiyo Mama Julia Morley (CBE), Mnyange wa Dunia wa sasa @suchaaata na Mnyage wa Afrika @hasset_dereje kujadiliana maendeleo ya sekta hiyo.

Rais Samia ameridhia Tanzania kuanza maandalizi ya kuwa mwenyeji wa shindano hilo mwaka 2027 uamuzi ambao utafungua mafanikio lukuki kwa nchini ikiwemo katika uendelezaji wa vipaji, sanaa na utalii na zaidi kukuza chapa (brand) ya nchi katika dunia hii iliyosheheni ushindani.

“Ukiondoa matukio ya awali yanayokwenda mwaka mzima, fainali pekee ya Unyange Duniani ambayo huhudhuriwa na takribani watu 5,000 ukumbini, tukio hilo kubwa duniani husomwa, hutazamwa na kufuatiliwa na watu zaidi ya bilioni diniani,” anasema Dkt. Hassan Abbasi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili mara baada ya kikao hicho muhimu akifafanua namna utalii utakavyonufaika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *