Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariTEC yabariki uchaguzi

TEC yabariki uchaguzi

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limebariki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, huku likikemea matukio ya utekaji na kupotea kwa watu.

Katika msisitizo wake kuhusu uchaguzi, TEC imewataka wananchi kuongozwa na dhamira safi, hai inayozingatia hofu ya Mungu na wasikubali kurubuniwa kwa vitisho.

Kauli hiyo imetolewa leo, Jumanne Oktoba 14, 2025 na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Amani ya TEC, Askofu Juda Ruwa’ichi katika hafla ya Maadhimisho ya Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania.

Amesema uchaguzi ni tukio la kikatiba na ndilo ambalo wananchi wanatarajiwa kuwapa waliowachagua dhamana ya kutawala na kuongoza nchi.

“Uchaguzi Mkuu ni tukio la kikatiba kwani hapo ndipo wananchi hutegemewa kuwapa waliowachagua dhamana ya kutawala na kuongoza nchi.

“Tanzania inapomkumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ni vema kutafakari kuhusu nchi na historia yake katika masuala ya Uchaguzi Mkuu,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu, amewataka wananchi kuongozwa na dhamiri safi,

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments