TECNO yawaasa vijana kuhusu teknolojia ya AI, yazindua CAMON 40

Vijana wameaswa kukumbatia na kuichangamkia teknolojia mpya ya Akili Bandia yaani AI kwani haikwepeki kwa ulimwenguwa sasa hivi.

Hayo yamesemwa na Mkufunzi wa kampuni ya TECNO, Jackline Saigero wakati wa uzinduzi rasmi wa simu mpya ya CAMON 40 JIjini Dar es Salaam ambayo ina uwezo mkubwa wa teknolojia ya AI.

“Teknoljia hii haikwepeki kabisa katika dunia ya sasa hivi kwa maana hiyo sisi kama TECNO tumeamua kuja na simu hii yenye uwezo mkubwa ulioboreshwa wa AI na ni matumaini yetu kuwa vijana wataitumia vizuri katika shughuli mbalimbali,” alisema

Amesema TECNO itaendelea kutoa bidhaa bora zinazokwenda na wajkati hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inaendeshwa na teknolojia ya kisasa ikiwemo ile ya AI na mahitaji ya upigaji picha ulio bora.

Uzinduzi huo wa CAMON 40 ulihusisha matoleo matatu ambayo ni pamoja na CAMON 40 Premier 5G, CAMON 40 Pro 5G, CAMON 40.

Alisema bidhaa hiyo tayari imeshazinduliwa katika masoko mengine yanayoongoza duniani kote ili kuhakikisha watumiaji, wakiwemo wale walioko Tanzania, wanapata bidhaa hiyo kwa urahisi katika maeneo yote ya kibiashara.

“Hii ni bidhaa yetu ambayo umeitoa hivi karibuni na ambayo ina ubora wa hali ya juu ikiwemo ya upigaji picha zenye ubora na huduma zingine za mawasiliano ya hali juu zaidi ikiwemo huduma za kisasa za AI,” alisema.

Alisema CAMON 40 Pro 5G ni bidhaa ya kipekee zaidi kutokana na kuwa na kamera ya kisasa aina ya 138 kutokaDXOMARK ambayo inashika nafasi ya kwanza katika orodha inayotolewa na taasisi ya Global Photography kwa simu ambazo bei yake ni chini ya Dola 600 na ndiyo simu ya kwanza kupokea tuzo Lebo ya simu janja bora zaidi kwa mwaka wa 2025.

“Mtiririko huu wa utoaji wa simu ana ya CAMON 40 unaonyesha harakati ambazo kampuni ya TECNO inaendelea nazo katika kuhakikisha wateja wanapta huduma bora haswa katika kipindi hii ambacho kua mahitaji kubwa ya huduma bora ikiwemo zil zinazohusiana na maswala ya Akili Mnembo (AI) na pigaji picha ulio bora zaidi”, alisema Mkufunzi huyo huku akiongeza, “Sifa kuu ya CAMON 40 ni uwezo wake wa kimapinduzi wa kupiga picha unaoendeshwa na huduma ya AI ambapo kupitia mfumo huo unawezesha upigaji wa picha zenye ubora zaidi na kuifanya kampuni ya TECNO kuendelea kuvuka mipaka ya kutoa bidhaa zenye kupiga picha zenye ubora kwa watumiaji wake”.

“Katika msingi wake, hali ya FlashSnap inayoendeshwa na AI inaunganishwa bila kiungo kingine chochote na kamera yenye nguvu na kitufe ambacho kikiguswa mara moja tu kinamwezesha mtumiaji kunasa kwa haraka zaidi”, alifafanua.

Aliendelea kusema kwa FlashSnap, AI huboresha uanzishaji wa kamera na upigaji picha mfululizo kwa ajili ya kunasa papo hapo, huku uchakataji wa fremu nyingi unaoendeshwa na AI hupunguza kelele na kuongeza maelezo kwa picha kali zaidi.

“Zaidi ya hayo, algoriti ya Best Moment AI huchanganua kwa akili ruwaza za mwendo, kubainisha kiotomatiki na kuchagua fremu bora zaidi ili kuhakikisha kunaswa kwa usahihi katika matukio yanayobadilika na kuwapa watumiaji taswira isiyo na kifani,” aliongeza

Kwa mujibu wa Jackline,CAMON 40 Premier 5G na CAMON 40 Pro 5G husukuma ubunifu wa upigaji picha unaoendeshwa na AI kwa viwango vipya. Kamera ya CAMON 40 Premier 5G’s 50MP Sony LYT-701 Ultra Night inakusanya mwanga zaidi ya asilimia 56.25% aina zingine za simu na hutoa picha safi zaidi kuliko kasi ya uono wa binadamu ya 200 blink kwa hatua za haraka.

Alifafanua kuwa CAMON 40 Premier 5G ina Kamera mpya ya Angle ya 50MP Ultra-wide, Kamera ya Simu ya 50MP Periscope na Kamera ya Mbele ya 50MP AF na ina uwezo wa kiwango cha 4K 60fps Pre-ISP Ultra Night ya Video yenye chip ya upigaji picha inayojitegemea, huku mfululizo mzima ukiwa na kamera mpya kabisa za selfie za mega-angle 50.

Kuhusu uimara alisema, “Pamoja na IP68 na IP69, ustahimilivu wa vumbi na maji, CAMON 40 Premier 5G, CAMON 40 Pro 5G, na CAMON 40 zimeundwa kuhimili hali mbaya aina yoyote wakati wa matumzi”.

Alibainisha kuwa simu ya CAMON 40 imeidhinishwa na IP66, kama bidhaa ya kuaminika na yenye uimara.

Wakati wa uzinduzi wa simu hiyo mpya, kampuni ya simu ya YAS ambayo imeingia makubaliano maalumu na TECNO ilitangaza faida mbalimbali watakazopata wanunzi wa simu hizo ikiwemo GB hadi 96 mwaka mzima bure.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa mawasiliano, wasanii wa Bongo Fleva na Movie, wachekeshaji na wasemaji wa vilabu vikubwa Tanzania- Simba na Yanga, Ahmed Ali na Ali Kamwe.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *