Timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu, Tembo Warriors, leo itaanza kampeni yake kwa kuvaana na Kenya katika mashindano ya CECAAF yanayofanyika Burundi.

Kocha Mkuu Ivo Mapunda amesema kikosi chake kipo tayari na wachezaji wote wana morali ya juu, huku nahodha Juma Kidevu akiahidi kupambana ili Tanzania ipate ushindi. Mashindano hayo yatahitimishwa Septemba 14.




