Tanzania imeandika historia mpya baada ya jana kuzinduliwa kwa kampuni ya The Diplomats, ambayo inalenga kutoa huduma za kitaalamu katika usimamizi wa matukio ya binafsi na ya kiserikali kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya protocol logistics.

Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Anthony William, alieleza kuwa The Diplomats itahakikisha wageni wa ngazi zote wanahudumiwa kwa viwango vya juu, huku ikiweka mkazo katika utoaji wa huduma jumuishi zinazohusisha:
Usimamizi wa wageni wa hadhi ya juu (VIP Guest Management).
Huduma za usafiri wa VIP.
Ulinzi wa karibu (Bodyguard Services).
Mapambo ya viwango vya kimataifa kwa matukio ya heshima.
Usimamizi wa shughuli maalum kwa kufuata taratibu za kidiplomasia.
Anthony William alibainisha kuwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo wamehitimu kutoka Chuo cha Diplomasia, huku wakiwa na uzoefu mkubwa kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.
“Tunajivunia kuwa kampuni ya kipekee inayoleta mapinduzi katika usimamizi wa matukio, tukitumia vifaa vya kisasa, teknolojia ya hali ya juu na wataalamu wenye weledi wa hali ya juu.
Pamoja na huduma zetu za kiwango cha kimataifa, tunahakikisha gharama zetu zinakuwa nafuu na rafiki kwa wateja wetu,” alieleza Anthony William.Kwa uzinduzi huu,
The Diplomats inaleta suluhisho jipya katika tasnia ya usimamizi wa matukio nchini Tanzania, huku ikitoa huduma zinazokidhi mahitaji ya sekta za umma na binafsi kwa weledi wa hali ya juu.