TPBRC yasisitiza upimaji afya kwa mabondia

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imetiliana saini mkataba wa miaka mitatu na Hospitali ya Hitech Sai kwa ajili ya huduma za afya kwa mabondia wake.

Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo, Emmanuel Saleh, alisema mkataba huo utahakikisha mabondia wanapimwa kabla na baada ya mapambano, jambo lililokuwa changamoto kwa muda mrefu.

Mtendaji Mkuu wa Hitech Sai, Sai Gean Cabral, alisema wameingia makubaliano hayo kwa kutambua umuhimu wa afya za mabondia na maendeleo ya mchezo huo nchini.
Aidha, hospitali hiyo pia inasaidia wachezaji wa michezo mingine kama kuogelea na kriketi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *