Bodi ya Ligi (TPLB) imesema ipo kwenye maandalizi ya msimu wa 2025/2026 kwa lengo la kuboresha zaidi ligi, baada ya mafanikio ya msimu uliopita.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa TPLB, Ibrahim Mwayela, amesema wanaendelea kupokea maoni ya wadau kuhusu kanuni mpya za ligi hadi Ijumaa, huku wakikamilisha kalenda ya matukio yote ya msimu.
Amezitaka klabu za Ligi Kuu kujiandaa vizuri na kupongeza juhudi zao kwenye usajili wa wachezaji bora ili kuimarisha ushindani wa ligi.