Waziri wa Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita amesema viwango vya juu vya Uwanja wa New Amaan Complex ndio sababu CAF imepeleka mechi za Kundi D la CHAN visiwani humo.

Michuano hiyo inaanza Agosti 2 kwa Taifa Stars kucheza na Burkina Faso jijini Dar, na mchezo wa kwanza Zanzibar utapigwa Agosti 5.
Zaidi ya kamera 42 za usalama, benchi maalum la viongozi wa CAF na miundombinu ya viwango vya kimataifa imekamilishwa. Rais wa ZFF Suleiman Jabir amewashukuru Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya michezo.