Ulinzi waimarishwa kesi ya Lissu, hakuna maandamano

Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, inayofanyika leo Mahakama ya Kisutu, kwa njia ya mtandao.

Katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, wameonekana Polisi wakipiga doria ili kudumisha ulinzi katika kesi hiyo, ambapo baadhi ya viongozi wa Chadema na wafuasi wao walipanga kuingia kwa wingi katika mahakama hiyo hali iliyohatarisha usalama na kuvuruga mwenendo wa kesi hiyo.

Jeshi la Polisi kwa kupitia Kamanda wake wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne Muliro, wameweka ulinzi katika kona mbalimbali za jiji ili kuhakikisha wananchi wote wanaendelea na shughuli zao kwa amani, bila kuvurugwa na mwenendo wa kesi hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *