Wadau wakutana kujadili mifumo endelevu ya usimamizi wa rasilimali maji

Wadau kutoka sekta mbalimbali wamekutana kujadili mifumo ya ushirikiano kwa usimamizi endelevu wa Rasilimali maji ndani ya maeneo ya kiuchumi ambapo mjadala umezingatia mbinu za uvumbuzi, ushirikiano wa sekta binafsi na umma, matumizi ya teknolojia, na sera endelevu ili kuhakikisha matumizi bora na uhifadhi wa rasilimali maji kwa maendeleo jumuishi.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na kuangalia namna bora ya kuweza kutumia maji kwa mara ya pili baada ya kutumika viwandani katika hali ya usalama na yasiweze kuathiri vyanzo vya maji vingine.

Akizungumza katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Sekta Binafsi, Aristides Robert Mbwasi, amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kulinda vyanzo vya maji ili kuchochea maendeleo ya Viwanda vyetu pasipo kuathiri jamii iliyotuzunguka.

“Hapa tunaangali namna salama ya maji yaliyotumika katika viwanda ili yasiweze kuleta athari kwa watumiaji wengine kama vile watumiaji wa mito na mabwawa na kulinda jamii kwa ujumla” amesema Mbwasi.

Awali, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassy, amesema katika kikao hiki kilichounganisha nchi mablimbali za Afrika na Ulaya ,lengo kubwa ni kujengeana uwezo na kuchangia uwezo na changamoto tunazokutana nazo katika kulinda vyanzo vya maji.

Amesema kuwa kwa upande kuwa Jiji la Dar es salaam mito imekuwa ikitumika kama mahala pa kuhifadhia taka mbalimbali ambapo hii imekuwa ikileta maradhi kwa wakazi na kuharibu vyanzo vya maji .

“Asilimia kubwa ya viwanda vya Dar es Salaam vimekuwa vikitumia maji ya Mto Ruvu kwa asili 70 hadi 80 kwa hiyo utupaji wa maji taka unaharibu hazina ya maji yaliyoko ardhini .hivyo tunaangalia namna ya kutumia teknolojia tuweze kumia majibyaliyotumika viwandani ili yaweze kurudi katika mzunguko ulio salama.” amesema .

Mkutano huu umewaleta pamoja washiriki kutoka nchi zinazotekeleza mpango wa GIZ NatuReS, zikiwemo Tanzania, Ethiopia, Zambia, na Afrika Kusini utakaofanyika kwa muda wa siku tatu Jijini Dar es salaam.

“Tonelamajilazimalihifadhiwe “

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *