
WANANCHI mbalimbali wamejitokeza kupata elimu kuhusu aina ya miamba na namna ya kupima sampuli za madini ya Metallic kwenye mashine ya XRF kwenye Banda la Tume ya Madini katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ Mashine hiyo ni maalumu inayotumika kupima madini ya metallic kwa njia ya MIONZI /X-RAY na kisha kukupa majibu kwa kukuonyesha kuwa madini hayo uliopima yana mchanganyiko wa madini gani, hukuonyesha madini yote yaliyomo ndani ya metal hiyo kwa asilimia tofauti tofauti.
Akitoa elimu hiyo kwa wananchi Afisa Maabara kutoka Tume ya Madini, Zuwena Mtoo amesema Madini yapo ya aina nyingi duniani lakini huwa hayakai yenyewe, lazima yanakuwa yamechanganyikana na aina mbalimbali nyingine za madini katika miamba.




Amesema, watu wanaonunua dhahabu ambao wanaogopa kutapeliwa kwa kuuziwa dhahabu feki wafike kwenye banda la Tume ya Madini kupata elimu namna ya kutambua miamba na madini mbalimbali pia wanaweza kupima Hereni, Mikufu ya dhahabu na silva katika banda, ameweza kushauri wananchi kuitumia fursa hii kufika katika maabara ya Tume madini iliyopo Msasani ili kubaini aina ya muamba.
Hii mashine ina kioo maalumu itakuonyesha kwenye kioo madini yalimo ndani mfano ukipima dhahabu baada ya mionzi kuscan itakuonyesha dhahabu ipo asilimia 11 na Silver ipo asilimia 89 sasa wewe ukiona hivi unajua moja kwa moja ulichouziwa ni feki ama si feki.




Amesema pia kuna mashine ya kupima sampuli za miamba kwa njia ya mionzi ambayo inatoa majibu ya ‘elements’ zote zilizomo kwenye huo mwamba na majina yake na wingi wake kwa kukuwekea asilimia yaani kama ni Kopa utaona itaandika “CU”….%, kama ni madini ya chuma itaandika “Fe”….% kama ni dhahabu ipo itaandika “Au”….%..
Aidha, Zuwena ametoa wito kwa wananchi wanaokuja sabasaba kutembelea banda la Tume ya Madini ili pia kujionea vito mbali mbali na kujifunza fursa zilizopo katika sekta ya madini.Kauli mbiu ya mwaka 2024 katika Maonesho ya Sabasaba ni ‘Tanzania Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji’.



