Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeHabariWaziri Kombo apokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule...

Waziri Kombo apokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule Angola

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa Domingos de Almeida da Silva Coelho, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kupokea Nakala za Hati hizo, Balozi Kombo amempongeza Mheshimiwa Domingos de Almeida da Silva Coelho kwa kuteuliwa kuiwakilisha Angola na amemuhakikishia ushirikiano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikalini kwa ujumla katika kipindi chote atakachohudumu hapa nchini.

Mhe. Kombo amesema Tanzania na Angola zimekuwa katika ushirikiano wa kidiplomasia na kirafiki kwa muda mrefu, tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1975, ambapo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya biashara na uwekezaji, mafuta na gesi, afya, ulinzi, madini, ufugaji wa Samaki, usafiri wa majini, utalii, miundombinu ya reli na Uchumi wa Buluu.

Kwa upande wake Mhe. Domingos de Almeida da Silva Coelho ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa Kindugu na kirafiki na kuhaidi kuendeleza ushirikiano huo kwa kuangazia fursa mpya za ushirikiano zaidi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments