Home Blog

Mganga wa tiba asili akamatwa kwa tuhuma za mauaji Kibaha

0

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Ally Shabani (29), mganga wa tiba asili na mkazi wa Makazi Mapya, Mlandizi wilayani Kibaha, kwa tuhuma za mauaji ya Juma Nyambihira.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), alisema tukio hilo lilifichuka baada ya ndugu wa marehemu kutoa taarifa ya kupotea kwake tangu Agosti 17. Taarifa hizo zilikabidhiwa Kituo cha Polisi Mlandizi mnamo Agosti 29, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ACP Msuya, baada ya taarifa hizo polisi walifungua jalada la uchunguzi na kuanza kufuatilia. Hatua hiyo ilimfikisha mikononi mwao mtuhumiwa Shabani, ambaye inadaiwa alikuwa akiishi na marehemu Juma akimpatia matibabu ya asili kutokana na tatizo la uoni hafifu.

Mwili Wapatikana Katika Shimo

Kamanda Msuya alieleza kuwa mnamo Septemba 3, wakati upelelezi ukiendelea, askari walifika nyumbani alipokuwa akiishi mtuhumiwa pamoja na marehemu kwa ajili ya upekuzi. Katika eneo hilo, walibaini uwepo wa tanuri la mkaa lililokuwa karibu na nyumba hiyo, ambapo kando yake kulionekana dalili za shimo.

“Baada ya kufukuliwa, tulibaini ndani ya shimo hilo ulikuwa mwili wa marehemu Juma Nyambihira,” alisema ACP Msuya.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Mtuhumiwa Kufikishwa Mahakamani

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtuhumiwa Ally Shabani atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika, huku likiendelea na hatua za uchunguzi ili kubaini undani wa tukio hilo.

BAVICHA yahoji matumizi ya mashtaka ya ugaidi

0

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Deogratias Mahinyila, ametoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kushirikiana kuhakikisha hali ya matumizi ya tuhuma za ugaidi dhidi ya wananchi inakomeshwa, akidai kuwa imekuwa ikitumiwa kuwabambikia watu kesi na kulichafua taifa.

Akizungumza leo katika ofisi za zamani za CHADEMA zilizopo Ufipa, Dar es Salaam, Mahinyila amesema kuwa utaratibu wa kuwasingizia na kuwabambikia wananchi kesi za ugaidi hauna haki na unaweza kuharibu taswira ya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Amedai kuwa kauli zinazotolewa kuhusu uwepo wa ugaidi nchini zinazua hofu miongoni mwa wananchi na zinaweza kudhoofisha uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine pamoja na kuathiri mazingira ya uwekezaji na utalii.

Mahinyila alisema taarifa zilizowahi kutolewa na Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 130 wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi, akisisitiza kuwa hali hiyo si jambo la kawaida kwa taifa na inapaswa kutazamwa kwa umakini.

Amehoji mantiki ya kauli zinazodai kuwa Tanzania haina ugaidi wakati kuna watu wanaoshikiliwa na kushtakiwa kwa makosa hayo, akidai kuwa baadhi ya watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka yasiyo ya kweli.

Aidha, ameeleza kuwa matumizi ya kesi za ugaidi yanaweza kuwa na athari kwa taswira ya Tanzania kimataifa, akidai pia kuwa yanaweza kuathiri maandalizi ya michuano ya AFCON kutokana na umuhimu unaowekwa na vyombo vya michezo duniani katika masuala ya haki za binadamu.

Samia begins official visit to Angola to deepen bilateral ties

0

President Samia Suluhu Hassan departed Tanzania on Friday for a two-day official working visit to Angola at the invitation of President João Lourenço, in a trip aimed at strengthening the longstanding relationship between the two countries.

During the visit, President Samia and President Lourenço will jointly inaugurate the Julius Kambarage Nyerere Referral Hospital in Luanda. The ceremony is expected to be attended by members of the late Mwalimu Julius Nyerere’s family, led by Mama Maria Nyerere, in recognition of his pivotal role in Africa’s liberation struggles.

Samia is also scheduled to hold bilateral talks with President Lourenço to discuss ways of expanding cooperation in key sectors and advancing issues of mutual interest between Tanzania and Angola.

As part of her programme, President Samia will attend a fundraising gala dinner organised by the spouses of African heads of state. The initiative seeks to raise funds for social and economic programmes that support the empowerment of women and young people across Africa.

According to a statement from the Presidency, the visit underscores the shared commitment of Tanzania and Angola to further strengthen their historic partnership, built during the struggle for the liberation of southern Africa and sustained through decades of close diplomatic cooperation.

Rais Samia akutana na Mama Maria Nyerere safarini Angola uzinduzi  Hospitali ya Nyerere

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai, 2026.

Mkuranga yapanua Shule kukabiliana na ongezeko la wanafunzi 

0

Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imeanza mkakati wa kujenga shule za msingi na sekondari za ghorofa kwa kutumia mapato ya ndani, hatua inayolenga kuongeza nafasi za wanafunzi na kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Waziri Kombo, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, Sh bilioni 1.7 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwandege, huku ujenzi wa Shule ya Sekondari Muungano ukiwa pia sehemu ya mpango huo.

Amesema Sh bilioni 2.1 zinatumika katika ujenzi wa Shule ya Msingi Mwandege ya ghorofa yenye vyumba 16 vya madarasa, huku mchakato wa ujenzi wa shule hiyo ukiendelea na mkandarasi akiwa tayari amepatikana kwa ajili ya shule ya sekondari.

Kombo amesema miradi hiyo itagharamiwa kupitia vyanzo vya mapato vya ndani, ikiwemo eneo la maegesho ya malori lenye ukubwa wa ekari 50 pamoja na mapato yatakayopatikana kupitia upangishaji wa eneo la bandari kavu.

Amesema Halmashauri itaendelea kusimamia na kuimarisha vyanzo hivyo ili kupata fedha za kugharamia ujenzi wa miundombinu ya elimu.

Kwa mujibu wa Kombo, ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mwandege unatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Shule hiyo kwa sasa ina vyumba 12 vya madarasa, hivyo kukamilika kwa jengo jipya kutaongeza nafasi kwa idadi kubwa ya wanafunzi.

Amesema ongezeko la wanafunzi linatarajiwa kuwa kubwa kutokana na mabadiliko ya sera ya elimu, hivyo Halmashauri imejipanga kuongeza madarasa na kujenga shule mpya, hususan katika kata za Mwandege, Vikindu, Vianzi na Mipeko ambazo zina idadi kubwa ya wanafunzi.

Kombo amewataka wazazi na wadau wa elimu kushirikiana na Serikali kwa kuchangia mahitaji madogo ya shule, akisema Serikali inaendelea kugharamia elimu bila ada pamoja na mahitaji makuu ya uendeshaji.

Amesema lengo ni kuhakikisha wanafunzi wote watakaofaulu wanapata nafasi ya kuendelea na Kidato cha Kwanza, huku ujenzi wa shule za ghorofa ukitarajiwa kuongeza uwezo wa Halmashauri kuhudumia ongezeko hilo la wanafunzi.

Minada ya ufuta yawaongezea wakulima mapato

0

Ubora wa ufuta unaozalishwa mkoani Pwani umeendelea kuchangia kuongezeka kwa bei katika minada, ambapo kilo moja imefikia Sh2,720 katika mnada wa sita uliofanyika katika Ghala Kuu la Kibiti.

Meneja wa CORECU Mkoa wa Pwani, Hamis Mantawela, amesema bei hiyo imeongezeka ikilinganishwa na mnada wa tano, ambapo kilo moja iliuzwa kwa bei ya juu ya Sh2,500.

Amesema katika mnada wa sita zaidi ya tani 400 za ufuta ziliuzwa, huku bei ya chini ikiwa Sh2,370 kwa kilo. Aidha, hadi kufikia mnada wa tano, zaidi ya Sh bilioni 30 zilikuwa zimelipwa kwa wakulima.

Mantawela amewataka wakulima na wadau ambao bado wana ufuta majumbani kuufikisha katika maghala ili uweze kushiriki katika minada rasmi, akisema hatua hiyo inaweza kuongeza ushindani na kuchochea bei kupanda zaidi.

Amesema minada hiyo inaendeshwa kwa uwazi kwa kuwa wakulima wanapata fursa ya kufuatilia mchakato wa mauzo, huku akibainisha kuwa hadi kufikia mnada wa tano hakukuwa na mkulima aliyekuwa akidai malipo.

Kwa upande wa bei kwa wilaya, Mkuranga iliongoza kwa Sh2,720 kwa kilo, ikifuatiwa na Kibiti Sh2,673.12, Bagamoyo, Chalinze na Kisarawe Sh2,616, huku Rufiji ikiuzwa kwa Sh2,554.32.

Afisa Rasilimali Watu wa TMX, Haikael Mkongo, amesema mfumo wa kidijitali umeongeza uwazi katika mauzo kwa kumwezesha mnunuzi na mkulima kufuatilia bei ya zao hilo kupitia simu.

Amewataka wakulima ambao bado hawajapeleka ufuta kwenye maghala kufanya hivyo ili wanufaike na mfumo wa minada ya kidijitali, ambao pia huokoa muda kwa wakulima na wanunuzi.

Ajali ya Makuyuni yaua sita, wengine wajeruhiwa

0

Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha basi la Kampuni ya Kandahari na malori mawili katika eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Julai 30, 2026, wakati basi la Kandahari lenye namba za usajili T 732 DRL, lililokuwa likitoka Kilimanjaro kuelekea Mpanda mkoani Katavi, lilipogongana uso kwa uso na semi-trela yenye namba T 727 EPW, iliyokuwa ikitoka Kahama kuelekea Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda, dereva wa basi alijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake katika eneo lenye kona, lakini kutokana na mwonekano hafifu wa barabara alikutana uso kwa uso na semi-trela iliyokuwa ikitokea upande wa pili.

Nguvu ya mgongano huo ilisababisha basi hilo kuharibika vibaya, huku baadhi ya abiria wakinaswa ndani ya gari. Dereva wa basi na abiria wengine walifariki katika ajali hiyo, huku majeruhi wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Lori jingine lenye namba T 757 DWV, lililokuwa likifuata semi-trela hiyo, lilipinduka wakati dereva wake alipokuwa akijaribu kukwepa ajali.

Vikosi vya uokoaji vikishirikiana na Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wasamaria wema vilifika eneo la tukio na kufanya operesheni ya kuwaokoa majeruhi, kutoa miili ya waliopoteza maisha na kuondoa magari yaliyoharibika.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika Barabara Kuu ya Arusha–Babati kwa saa kadhaa wakati shughuli za uokoaji na usafishaji wa barabara zikiendelea.

Hadi taarifa hii inaandaliwa, Jeshi la Polisi lilikuwa halijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi kamili ya majeruhi, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali na kuthibitisha takwimu za waathirika.

Rais Samia asisitiza maridhiano kuelekea maboresho ya Katiba

0

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendeleza maridhiano ya kisiasa nchini kuelekea hatua za maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Katika kuyatimiza hayo, ameahidi kuendeleza majadiliano na vyama vya siasa ili kujenga mwafaka kuhusu masuala muhimu ya Taifa.`

Rais Samia ameyasema hayo Julai 30, 2026 alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa nchini katika mkutano uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, amerejea maridhiano ya Zanzibar, akisema Serikali inaendelea na maandalizi ya hatua zinazofuata za mapitio ya Katiba na kwamba kila hatua itazingatia misingi ya sheria na maslahi mapana ya Taifa.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa angalau mara tatu kwa mwaka kwa lengo la kuimarisha mazungumzo, kujenga uelewano na kutafuta suluhu za masuala yanayohusu maendeleo ya nchi.

Mbali na masuala ya siasa, Rais Samia pia amezungumzia hali ya uchumi wa nchi akisema umeendelea kukua kwa asilimia sita mwaka uliopita, huku ukuaji wa asilimia 6.3 ukitarajiwa mwaka huu.

PPAA yawaelekeza wazabuni kutumia Mfumo wa NeST

0

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewahimiza wazabuni na wadau wa ununuzi wa umma kutumia Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) kuwasilisha malalamiko na rufaa zao PPAA pindi wanapoona hawakutendewa haki katika michakato ya ununuzi wa umma.

Akizungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa Kongamano la kumi la ununuzi wa Umma la mwaka 2026 linaloendelea Jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma PPAA, Nelson Kessy amesema kuanza kwa matumizi ya Moduli hiyo kuna faida nyingi kama vile kuokoa muda na gharama.

“Faida nyingine za wazabuni na taasisi nunuzi kutumia moduli ni pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni, na kuongeza ufanisi katika utoaji wa uamuzi,” amesema Kessy

Kessy ameongeza kuwa Mamlaka ya Rufani inawaelekeza wazabuni wote wa ndani na nje ya nchi kutumia Moduli ya kuwasilisha Malalamiko na Rufaa kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake pindi wanapoona hawakutendewa haki katika zabuni walizoomba.

Katika hatua nyingine, Kessy amesema kuwa PPAA inatoa huduma ya Mkutano kwa njia ya Mtandao “Video Conference” ambapo hutumika kusikiliza mashauri ya wazabuni walioshindwa kufika moja kwa moja katika Ofisi za PPAA kwa ajili ya kusikiliza mashauri yalilowasilishwa mbele yake.

Huduma ya Mkutano kwa njia ya Mtandao imetoa fursa ya kuwasikiliza wazabuni walioshindwa kufika PPAA kutokana na sababu mbalimbali na kuiwezesha Mamlaka ya Rufani kutekeleza jukumu lake la msingi la utatuzi wa migogoro itokanayo na michakato ya ununuzi wa Umma. 

“Tangu kuanza kwa matumizi ya ‘video conference’ tayari PPAA imewasikiliza wazabuni mbalimbali kutoka katika mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria, Poland, India na China,” amesema Kessy. 

Kadhalika, Mamlaka ya Rufani inatarajia kuunganisha Moduli ya Malalamiko na Rufaa na mfumo wa Mahakama ya Tanzania ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha matumizi ya teknolojia katika sekta ya ununuzi wa umma. 

Naye mzabuni Peter Sarungi kutoka makundi maalum alisisitiza sekta ya makundi maalum ipewe kipaumbele zaidi katika uombaji wa zabuni na kufuatilia taasisi zilizotangaza zabuni ili wapewe taarifa kama wamepata zabuni au la ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwemo kutumia Moduli ya PPAA. 

Matumizi rasmi ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST yalianza mwezi Februari, 2025.

CRDB Foundation Trains SIDO, ZEEA Officials to Strengthen MSME Support Services

0

In an effort to enhance the capacity of institutions supporting entrepreneurs in Tanzania, CRDB Bank Foundation has conducted specialised training for officials from the Small Industries Development Organization (SIDO), the Zanzibar Economic Empowerment Agency (ZEEA), and local government authorities from Mwanza, Tanga and Pemba regions.

The training is part of the implementation of the Inclusive Financial Services for Women and Youth-led MSMEs (IncluCities Project SASA), which aims to increase access to financial services and development opportunities for women and young entrepreneurs.

Opening the three-day training, CRDB Bank Head of Agribusiness Services, Shaaban Maregesi, said the programme was organised following an assessment that identified areas requiring further improvement despite the institutions having experienced staff and strong operational systems.

He mentioned key areas requiring enhancement as entrepreneurship advisory services, financial management, small and medium enterprise (SME) appraisal, customer care, and the use of digital systems in service delivery.

“There is a great opportunity to continue strengthening the capacity of these institutions so they can provide more efficient services to citizens and help them grow their businesses,” Maregesi said.

The IncluCities Project SASA is implemented through a partnership between CRDB Bank Foundation and international development organisation Enabel. So far, the project has reached more than 200 beneficiaries in Tanga, Mwanza and Pemba, while over 50 entrepreneurs have benefited from business support capital worth more than 400 million Tanzanian shillings.

Maregesi said CRDB Bank Foundation’s goal is to ensure institutions serving women and youth have greater capacity to support them in joining the formal economy, expanding their businesses and accessing financial services more easily.

“The success of women and youth entrepreneurs largely depends on the ability of institutions around them to provide quality, appropriate and timely services. This is why we continue investing in strengthening the capacity of these institutions,” he said.

Participants are expected to gain skills in six key areas, including entrepreneurship development, financial management, good governance and institutional leadership, SME appraisal, customer service, and the use of digital technologies to improve service delivery.

According to CRDB Bank Foundation, its partnership with SIDO, ZEEA, local government authorities and Enabel aims to create a better environment for entrepreneurs, increase employment opportunities and promote inclusive economic growth in Tanzania.

Beyond this project, the foundation continues to work with the government through various empowerment programmes, including the Inuka and Zanzibar Blue Economy initiatives, as well as providing loan guarantees for entrepreneurs trained through SIDO.

The training is expected to improve services offered by partner institutions, strengthen collaboration among stakeholders, and empower women and youth to effectively utilise available economic opportunities to grow businesses, create jobs and increase income.

CRDB Foundation yawezesha taasisi kukuza wajasiriamali

0

Katika jitihada za kuimarisha uwezo wa taasisi zinazowahudumia wajasiriamali nchini, CRDB Bank Foundation imeendesha mafunzo maalumu kwa maafisa wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) na watendaji wa Serikali za Mitaa kutoka mikoa ya Mwanza, Tanga na Pemba.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Inclusive Financial Services for Women and Youth-led MSMEs (IncluCities Project SASA) unaolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha na fursa za maendeleo kwa wanawake na vijana wajasiriamali.

Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wakulima wa Benki ya CRDB, Shaaban Maregesi, amesema mafunzo hayo yameandaliwa kufuatia tathmini iliyobaini kuwa, licha ya taasisi hizo kuwa na watumishi wenye uzoefu na mifumo imara ya utendaji, bado kuna maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni ushauri wa ujasiriamali, usimamizi wa fedha, tathmini ya biashara ndogo na za kati (SME Appraisal), huduma bora kwa wateja pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali.

“Kuna fursa kubwa ya kuendelea kuimarisha uwezo wa taasisi hizi ili ziweze kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi na kuwasaidia kukuza biashara zao,” amesema Maregesi.

Mradi wa IncluCities Project SASA unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya CRDB Bank Foundation na taasisi ya maendeleo ya kimataifa ya Enabel. Hadi sasa umewafikia zaidi ya wananchi 200 katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Pemba, huku zaidi ya wajasiriamali 50 wakinufaika na mitaji wezeshi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400.

Maregesi amesema lengo la CRDB Bank Foundation ni kuhakikisha taasisi zinazotoa huduma kwa wanawake na vijana zinakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwawezesha kuingia katika uchumi rasmi, kukuza biashara zao na kupata huduma za kifedha kwa urahisi.

“Mafanikio ya wanawake na vijana wajasiriamali yanategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa taasisi zinazowazunguka kuwapa huduma bora, sahihi na kwa wakati. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza katika kuzijengea uwezo taasisi hizi,” amesema.

Washiriki wa mafunzo hayo wanatarajiwa kupata ujuzi katika maeneo sita muhimu ambayo ni maendeleo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha, utawala bora na uongozi wa taasisi, tathmini ya biashara ndogo na za kati, huduma kwa wateja na matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kuboresha utoaji wa huduma.

Kwa mujibu wa CRDB Bank Foundation, ushirikiano wake na SIDO, ZEEA, Serikali za Mitaa na Enabel unalenga kujenga mazingira bora kwa wajasiriamali, kuongeza ajira na kukuza uchumi jumuishi nchini.

Mbali na mradi huo, taasisi hiyo imeendelea kushirikiana na Serikali kupitia programu mbalimbali za uwezeshaji, ikiwemo Inuka na Uchumi wa Buluu Zanzibar, pamoja na kutoa dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wanaopata mafunzo kupitia SIDO.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi washirika, kuongeza ushirikiano kati yao na kuwawezesha wanawake na vijana kutumia kikamilifu fursa za kiuchumi zilizopo kwa ajili ya kukuza biashara, ajira na kipato.