Yanga karibu kufunga pazia la usajili

Klabu ya Yanga imetangaza kuwa imebakiza kumsajili mchezaji mmoja tu ili kukamilisha dirisha la usajili wa wachezaji wapya kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alisema zoezi la usajili limeenda vizuri, na wiki hii ndilo litakuwa hitimisho.

“Tunafunga kazi ya usajili wiki hii, tumebakiza mchezaji mmoja tu. Tayari tumeshawatangaza wale tunaowaacha na waliomaliza mikataba, na tutamalizia na wale tuliowaongeza pamoja na wapya,” alisema Kamwe.

Aliongeza kuwa Yanga itaanza kambi ya maandalizi kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itafanyika ndani ya nchi, na baadaye wataelekea Rwanda kwa ajili ya kushiriki tamasha la Rayon Sports. Baada ya hapo, kikosi hicho kitaelekea nje ya Tanzania kwa kambi ya pili ya maandalizi ya msimu.

Mechi dhidi ya Rayon Sports itapigwa Uwanja wa Amahoro, Kigali, kama sehemu ya tamasha la ‘Rayon Sports Day’.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *