Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeBiasharaYas na Mixx Wazindua Duka Jipya Dar Village Mall, Waimarisha Huduma kwa...

Yas na Mixx Wazindua Duka Jipya Dar Village Mall, Waimarisha Huduma kwa Wateja

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya Yas, kwa kushirikiana na Mixx, leo imezindua duka jipya katika Dar Village Mall, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kusogeza huduma karibu zaidi na wateja, sambamba na kuunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Uzinduzi huo umefanyika wakati dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, yenye kaulimbiu ya mwaka huu “Mission Possible”, ikiakisi dhamira ya Yas kuwa mshirika wa kweli wa Watanzania katika safari yao ya mafanikio ya kidijitali.

Kupitia duka hilo jipya, Yas inalenga kutoa huduma bora na za kisasa zaidi kwa wateja wake, ikiwemo msaada wa papo kwa papo, ushauri wa kitaalamu, pamoja na fursa ya kujifunza kwa vitendo namna teknolojia za 4G na 5G zinavyoweza kuboresha maisha ya kila siku.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Yas, Bw. Jorge Soto, alisema kampuni hiyo imejipanga kuendelea kuchochea fikra bunifu miongoni mwa wafanyabiashara, wajasiriamali na watumiaji wa huduma za kidijitali ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

“Kupitia maduka kama haya, tunaleta huduma karibu zaidi na wateja wetu, tukiwapa nafasi ya kugusa, kuona na kuelewa uwezo wa teknolojia za kisasa ambazo ni msingi wa maendeleo ya kidijitali nchini,” alisema Bw. Soto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas na Mixx, Bi Mwangaza Matotola, alisema wiki ya huduma kwa wateja ni fursa muhimu ya kuimarisha mahusiano na wateja, na kuwasaidia kunufaika zaidi na fursa za kidijitali.

“Lengo letu ni kuhakikisha kila mteja anahisi thamani yake. Kupitia duka hili jipya, tutawawezesha Watanzania kufikia huduma kwa urahisi na kwa uzoefu bora zaidi,” alisema Bi Matotola.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mixx, Bw. Arnold Ngarashi, alisema uzinduzi wa Yas Store unaakisi dhamira ya Mixx by Yas ya kuleta mageuzi ya huduma za kifedha kwa njia za kidijitali, na kuhakikisha huduma hizo zinapatikana kwa urahisi zaidi kwa Watanzania wote.

“Kupitia Mixx by Yas, tunalenga kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kuwapa suluhisho bunifu za kifedha zinazoendana na mahitaji yao ya kila siku. Uzinduzi wa Yas Store ni sehemu ya safari yetu ya kuboresha namna Watanzania wanavyopata, kutumia na kufurahia huduma za kifedha na mawasiliano kwa pamoja chini ya mfumo mmoja wa kidijitali,” alisema Bw. Ngarashi, na kuongeza kuwa “Tunataka kila mteja anapokutana na Mixx by Yas, ahisi urahisi, ubunifu na usalama unaoleta mabadiliko chanya katika maisha yake.”

Uzinduzi wa Yas Store katika Dar Village Mall unatarajiwa kuwa mwanzo wa mtandao mpana wa maduka ya kidijitali yatakayofunguliwa katika mikoa mbalimbali nchini, yakihimiza matumizi ya teknolojia bunifu na huduma rafiki kwa wateja.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments