Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeMichezo⚽ CECAFA yamteua Mganda kuwa Kaimu CEO mpya

⚽ CECAFA yamteua Mganda kuwa Kaimu CEO mpya

Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limemteua Mganda Jean Sseninde kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya, kuchukua nafasi ya Auka Gecheo wa Kenya.

Sseninde, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Uganda, alikuwa Meneja wa Maendeleo ya Soka la Wanawake CECAFA.

Kaimu Rais wa CECAFA, Alexandre Muyenge, amesema anaimani uteuzi huo utaongeza kasi ya maendeleo ya soka katika ukanda huo.

Uchaguzi mkuu wa baraza hilo unatarajiwa kufanyika mapema mwakani.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments