Bondia Ibrahim Mafia ameapa kumpiga Alvin Camique wa Ufilipino katika pambano la “Knock Out ya Mama” litakalofanyika leo Viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam.
“Nimemsoma vizuri, hana uwezo mkubwa. Nimejiandaa kumpa somo ulingoni,” alisema Mafia kwa kujiamini.
Bondia Yohana Mchanja naye atapanda ulingoni dhidi ya Aldri Portililo kutoka Venezuela, akiahidi “kutoa kazi na utu.”
Meneja wa Mafia Boxing Promotion, Anathol Wannah, alisema maandalizi yote yamekamilika na mashabiki wanatarajiwa kushuhudia burudani ya kipekee kutoka kwa mabondia wa ndani na nje.