Waziri wa SMZ atembelea banda la PSSSF Nanenane Zanzibar

Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shaib Kaduara ametembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Dole Kizimbani, Zanzibar na kuelezwa namna ambayo sasa wanachama wanapata huduma za Mfuko zote kupitia simu janja.

Akitoa maelezo kwa Kaduara, Meneja wa PSSSF, Zanzibar, Jafari Meraji, amemueleza Waziri kuwa, Wanachama na wananchi wanaotembelea kwenye banda hilo, wanapatiwa elimu ya Hifadhi ya Jamii, lakini pia wanachama wanapatiwa huduma zikiwemo za kupata taarifa ya michango yao, taarifa za Mafao, lakini pia taarifa za uwekezaji.

“Mhe. Waziri kwa sehemu kubwa huduma zetu kwa sasa tunazitoa kupitia mtandao, hivyo wanachama wetu wanapofika hapa pia tunawaunganisha na PSSSF Member Portal, ambapo mwanachama anapojiunga kupitia simu janja, anaweza kupata huduma zote zitolewazo na Mfuko akiwa mahali popote bila ya kuhitaji kutembela ofisi za Mfuko,” alisema Meraji.

Mwanachama akielimishwa kuhusu huduma za PSSSF
Timu ya PSSSF inayotoa huduma maonesho ya Nanenane Zanzibar.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *