Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariPolisi Geita: Dumisheni amani mitandaoni

Polisi Geita: Dumisheni amani mitandaoni

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limewataka viongozi wa makundi ya mitandao ya kijamii, hususan WhatsApp, kudhibiti usambazaji wa taarifa za uchochezi na uvunjifu wa amani.

Wito huo umetolewa Desemba 8, 2025 na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SACP Safia Jongo, alipoungana na Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net) kutoa msaada katika Kituo cha Afya Nyankumbu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Kamanda Jongo amesema mitandao ya kijamii, ikiwemo makundi ya WhatsApp, isinageuzwe majukwaa ya kusambaza chuki, vitisho, taarifa za upotoshaji na unyanyasaji wa kidijitali dhidi ya wanawake na wasichana. Alibainisha kuwa wasimamizi na wanachama wa makundi hayo wana jukumu muhimu la kudhibiti maudhui yanayokiuka maadili, sheria na yanayoweza kuchochea uvunjifu wa amani.

“Wasimamizi wa makundi ya WhatsApp na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuhakikisha majukwaa haya hayatumiki kufanya uhalifu au kuendeleza ukatili wa kijinsia. Ni wajibu wa kila mmoja kudhibiti taarifa hatarishi zinazoweza kuathiri amani,” amesema Jongo.

Ameongeza kuwa TPF-Net inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kupambana na ukatili unaofanywa kupitia majukwaa ya kidijitali, pamoja na kuhamasisha wananchi kutoa taarifa mapema wanapokutana au kushuhudia vitendo vya ukatili.

Aidha, Kamanda Jongo amewataka wananchi kuepuka vitendo vyenye viashiria vya vurugu, uhalifu na uvunjifu wa amani, huku akisisitiza umuhimu wa kukomesha aina zote za ukatili, hasa ule unaolenga wanawake na wasichana kupitia mitandao ya kijamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments