Friday, December 5, 2025
spot_img
HomeAfyaDk. Jafari: Watoa huduma tumieni lugha ya heshima kwa wagonjwa

Dk. Jafari: Watoa huduma tumieni lugha ya heshima kwa wagonjwa

Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya afya na Mbunge wa Jimbo la Busanda, Dk. Jafari Seif, amewataka watumishi wa afya kote nchini kuhakikisha wanatumia lugha ya heshima, upole na tabasamu wanapotoa huduma kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya.

Dk. Jafari ametoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea Kituo cha Afya cha Nyarugusu kilichopo Kata ya Nyarugusu, Jimbo la Busanda, Wilaya ya Geita, ambako alizungumza na watumishi wa kituo hicho juu ya umuhimu wa huduma bora zenye utu na ukarimu.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha huduma za afya kupitia ujenzi na ukarabati wa vituo, zahanati na miundombinu mbalimbali. Hata hivyo, amesisitiza kuwa maboresho hayo hayawezi kuwa na tija endapo watoa huduma hawatatumia lugha nzuri na kuwakaribisha wagonjwa kwa tabasamu.

“Hata kama tunajenga na kukarabati vituo, bado nyinyi watoa huduma mna wajibu wa kumhudumia mgonjwa kwa lugha safi, si lugha chafu,” amesema Dk. Jafari.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Fred Feliasianj, amesema wamefurahishwa na ziara ya Naibu Waziri na kubainisha kuwa kituo hicho kinahudumia wananchi wengi, hivyo kinahitaji maboresho zaidi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments