Wakazi wa Dar es Salaam wametoa wito wa kuzingatiwa na kudumishwa kwa amani nchini, wakisema ndio msingi wa ustawi wa maisha ya watu.
Wamesisitiza matishio ya vurugu yanavyoathiri shughuli za kiuchumi na biashara, hasa Desemba ambayo mara nyingi huwa mwezi wenye faida.
Mfanyabiashara wa vifaa vya magari, Hamis Kiloko ni mmoja wa wakazi hao, amesema ni muhimu kudumisha amani na kuepuka vurugu, kwani zinaathiri biashara yake.




