Serikali ya Tanzania na Marekani zimekubaliana kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu baina ya mataifa hayo.
Hatua hiyo, imefikiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo nchini humo alikokutana na viongozi mbalimbali wa Marekani.
Balozi Kombo ameanza ziara hiyo, Jumatatu Desemba 15, 2025 na kukutana na viongozi mbalimbali wa bunge na Serikali ya Taifa hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania mjini Washintong, Serikali hizo zimekubaliana mambo kadhaa ya uimarishaji mahusiano hayo.
Pia, Kamati ya Bunge la Marekani, imepokea mwaliko wa kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.
Miongoni mwa viongozi aliokutana nao ni Mbunge wa Florida kupitia Chama cha Republican, Brian Mast, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani.






