Wednesday, December 17, 2025
spot_img
HomeHabariWazamiaji wasababisha Marekani ibane Viza kwa Watanzania

Wazamiaji wasababisha Marekani ibane Viza kwa Watanzania

Serikali ya Marekani imesema itadhibiti utoaji wa visa kwa Watanzania wanaokwenda nchini humo kutokana na raia wake kukithiri kwa kukaa zaidi ya muda uliopaswa (overstay).

Kwa mujibu wa tamko la Rais Donald Trump wa Marekani, Tanzania imetajwa katika muktadha wa tahadhari, tofauti na mataifa mengine 23 ambayo yamewekewa vikwazo vya kuingia Marekani kwa sababu tofauti.

Kutokana na tangazo hilo la Marekani, Watanzania wataokuwa na uhakika wa kupata viza kuingia katika taifa hilo lenye nguvu duniani ni wale watakaokidhi vigezo na masharti vilivyowekwa na serikali hiyo.
Taarifa ya Serikali ya Marekani imetaja makundi kama vile wanamichezo, wanadiplomasia na watu ambao uingiaji wao unalinda maslahi ya taifa hilo na wale ambao watakidhi vigezo vingine ndiyo watakaopewa viza hizo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments