Wednesday, December 17, 2025
spot_img
HomeElimuWaziri Mkenda asifu Mradi wa HEET Mloganzila

Waziri Mkenda asifu Mradi wa HEET Mloganzila

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema maendeleo yanayoendelea katika Kampasi ya Mloganzila ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ni matokeo ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu hiyo, Prof. Mkenda alisema mradi huo unatekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kupanua elimu ya juu na huduma za afya kwa kujenga vituo vipya vya umahiri nje ya kampasi zilizopo.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Apollinary Kamuhabwa, alisema Mradi wa HEET katika Kampasi ya Mloganzila unagharimu Dola za Kimarekani milioni 45.5, ambapo dola milioni 30 zinatumika moja kwa moja Mloganzila. Ujenzi huo unahusisha mabweni ya wanafunzi, maabara za kisasa zipatazo 20, maktaba, jengo la utawala na kumbi za mihadhara.

Alisema ujenzi ulioanza Desemba 2024 umefikia kati ya asilimia 50 hadi 70, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2026. Kampasi hiyo pia tayari ina Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu, huku ujenzi wa Hospitali ya Magonjwa ya Damu ukitarajiwa kuanza mwaka ujao.

Mradi huo unalenga kuifanya Mloganzila kuwa mji wa kitaaluma wa tiba, kuongeza ubora wa mafunzo, tafiti na uzalishaji wa wataalamu wabobezi wa afya kwa Tanzania na Afrika Mashariki.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments