Tuesday, March 31, 2026
spot_img
HomeMichezoOsimhen asimulia maumivu ya kusaidia rafiki asiyeridhika

Osimhen asimulia maumivu ya kusaidia rafiki asiyeridhika

SIYO kila msaada unaotolewa kwa moyo hupokelewa kwa shukrani—hilo ndilo somo alilolipata mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, kutoka kwa mmoja wa marafiki zake wa utotoni.

Osimhen aliwahi kufunguka kuhusu tukio lililomuumiza baada ya kumsaidia rafiki yake kifedha, lakini badala ya kushukuru, rafiki huyo aliona kiasi alichopewa hakikutosha.

Alieleza kuwa alikuwa na desturi ya kumtumia rafiki yake huyo fedha mara kwa mara. Siku moja, rafiki huyo alimfuata na wazo la kuanzisha biashara, jambo lililomfanya Osimhen kuamua kumsaidia bila kusita kwa kumtumia euro 5,000 (takribani Sh milioni 14.8 za Kitanzania).

“Nilikuwa namtumia pesa mmoja wa marafiki zangu wa utotoni, lakini siku moja aliniambia kuhusu biashara aliyotaka kuanzisha. Nikamtumia euro 5,000, lakini hakushukuru,” alisema Osimhen.

Hata hivyo, kilichomuuma zaidi ni majibu aliyopokea kutoka kwa rafiki huyo, ambaye aliona kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na mapato ya Osimhen anayodaiwa kupata akiwa Ulaya.

“Aliniambia amesoma kuwa napata euro milioni 1 kwa wiki, hivyo alitarajia euro 50,000 (takribani Sh milioni 148.7),” aliongeza.

Osimhen alisema alikasirishwa sana na hali hiyo kiasi cha kutamani kufuta muamala huo, lakini haikuwezekana. Alisisitiza kuwa kiwango hicho cha fedha ambacho wengine wanaweza kudharau, kwa mazingira ya Nigeria ni kikubwa na kinaweza kubadilisha maisha ya mtu.

“Euro 5,000 Ulaya inaweza kununua jozi moja tu ya viatu vya gharama, lakini Nigeria ni pesa nyingi sana. Hakuna aliyewahi kunitumia hata dola 1 kabla sijafika Ulaya. Nilihangaika mchana na usiku, niliuza maji ya chupa barabarani,” alisema.

Kwa kumalizia, Osimhen alitoa ujumbe mzito kwa jamii, akihimiza watu kuthamini msaada wanaopata badala ya kuwa na matarajio makubwa yasiyo na shukrani.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments